English English Swahili Swahili

THE REVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR

Zanzibar Bureau of Standards

ISO 9001: 2015 CERTIFIED

Standards | Quality | Life

aerial photography of village near body of water

TAARIFA JUU YA UANZISHWAJI WA VIWANGO VYA HUDUMA ZA UTALII TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR ILI KUBORESHA HUDUMA KWA MUJIBU WA VIWANGO VILIVYOWEKWA

Zanzibar, 17 februari, 2022. Taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa Sheria ya Viwango ya Zanzibar namba 1 ya mwaka 2011. ZBS imeanza hatua za utekelezaji wa kazi zake rasmi mwaka 2012 ikiwa na jukumu la msingi la kuandaa viwango vya bidhaa na huduma pamoja na kusimamia matumizi ya viwango katika bidhaa na huduma. Lengo kuu la kazi za ZBS ni kulinda afya na usalama wa mtumiaji, kulinda mazingira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Taasisi ya viwango Zanzibar katika hatua zake zake za uandaaji wa viwango imenza kuanda viwango vya huduma za utalii ili kuendana na kasi ya maendeleo ya kuendeleza uchumi kupitia utalii ambapo itakuwa chachu ya maendeleo halikadhalika kufanya kazi kwa ufanisi katika kutoaji wa huduma hii ya utalii, zbs imeweza kuanda viwango vifuatavyo :- ZNS 110:2018 Tour operators and travel agents- Code of practice ZNS 112:2018 Hotels, restaurants and related establishments — Code of practice ZNS 113:2018 Tourism related water sports activities with in Zanzibar’s territorial water — requirement ZN ZNS 113:2018 Tourism related water sports activities with in Zanzibar’s territorial water — requirementS 114:2018 Tourism services — Beach safety ZNS 114:2018 Tourism services — Beach safety ZNS 297: 2020 Tourist service vehicles — Code of practice ZNS 298: 2020 Motor vehicle rental operations — Requirements

VIWANGO VILIVYOPO KATIKA HATUA YA MAANDALIZI Viwango vinne vipo katika hatua za maandalizi katika hatua ya maoni kwa umma, viwango hivyo ni:- TCD 302 responsible tourism – requirement TCD 303 tour guiding services- requirements TCD 301 requirement for snorkelling excursions TCD 300 site and attractions – general requirement Nakala za viwango hivi ziko katika hatua ya zimeshasambazwa kwa wadau kwa ajili ya kukusanya maoni na pia zinapatikana katika tovuti ya taasisi www.zbs.go.tz

Taasisi ya Viwango Zanzibar inahakikisha bidhaa zinazoingia nchini na zinazozalishwa ndani zinakuwa katika viwango vinavyotakiwa kukidhi ubora uliokusudiwa na kubaki salama kwa ajili ya matumizi kwa wananchi na mazingira yetu. Hivyo, shughuli zetu kuu zitahakikisha na kuzingatia viwango na ubora wa bidhaa ili kuweka maisha salama kwa watumiaji.” halikadhalika “Zbs imejitolea kusaidia na kuwaunga mkono wadau wote, ikiwa ni pamoja na watoaji wa huduma za utalii ikiwemo mahoteli na taasisi mbalimbali katika shughuli zao na upatikanaji wa masoko. Na kukuza uchumi, tunalenga kuifanya ZBS kuwa miongoni mwa Taasisi zinazoongoza katika ukanda huu na Afrika.

Taasisi ya viwango Zanzibar inasisisitiza mashirikiano na taasisi zote za Serekali zinazosimamia maendeleo ya huduma za utalii ili kuweza kusaidia kufikia malengo ya maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.
S.L.P 1136,
NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225
Barua pepe: info@zbs.go.tz

Previous PRESS RELEASE ZBS AND TMEA