English English Swahili Swahili

Zanzibar Bureau of Standards

ISO 9001: 2015 Certified

Standards | Quality | Life

TAARIFA YA UANGAMIZAJI WA BIDHAAA YA PIPI ILIYOCHINI YA KIWANGO

Taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa Sheria ya Viwango ya Zanzibar namba 1 ya mwaka 2011. ZBS imeanza hatua za utekelezaji wa kazi zake rasmi mwaka 2012 ikiwa na jukumu la msingi la kuandaa viwango vya bidhaa na huduma pamoja na kusimamia matumizi ya viwango katika bidhaa na huduma. Lengo kuu la kazi za ZBS ni kulinda afya na usalama wa mtumiaji, kulinda mazingira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Katika kuhakikisha kwamba bidhaa zinazozalishwa ndani ya Nchi zinakidhi ubora wa viwango husika pamoja na kupata Udhibiti Ubora wa bidhaa, ZBS inahakikisha utekelezaji wa majukumu yake unaendana na sheria na kanuni ya viwango ya mwaka 2011 ambayo inaipa fursa ya kutoa maelekezo juu ya uangamizi wa bidhaa mbali mbali ambazo baada ya kufanyika uchunguzi wa kina bidhaa hizo ikiwa zimegundulika kuwa zipo chini ya viwango hatua za uangamizi hufanyika kwa mujibu wa sheria ya viwango katika kifungu cha 19. Baada ya hatua za ukaguzi uliofanyika tarehe 4 januari 2022 wa bidhaa zilizoingizwa nchini mnamo tarehe 30-11-2021, iliizuia bidhaa ya pipi yenye jina la SUPER CANDY iliyotoka nchini CHINA na kuingia nchini zanzibar chini ya kampuni ya YIWU TRADING COMPANY LTD. Bidhaa hiyo ilishindwa kufikia kiwango kilichowekwa cha ZBS –ZNS 175; 2017.

Baada ya taratibu za uchunguzi wa kimaabara bidhaa imegundulika kuwa na sababu iliyopelekea kuangamizwa ikuwa na kiwango kikubwa cha moisture,amabayo ni kuengezeka kwa unyevunyevu katika bidhaa hiyo. ‘Moisture constant’ ni unyevunyevu ambao katika bidhaa unatakiwa kuwa na wastani usiozidi wala kupungua katika kiwango maalum kilichowekwa, unyevunyevu huo kwenye chakula hupelekea kuibuka kwa vimelea ambavyo vitapelekea madhara makubwa kwa mtumiaji wa bidhaa hiyo hata kuhatarisha maisha.

Jumla ya maboksi mia mbili [200] ambayo yameangamizwa ya bidhaa hiyo ya SUPER CANDY.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.
S.L.P 1136,
NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225
Barua pepe: info@zbs.go.tz

Previous PRESS RELEASE ZBS AND TMEA