English English Swahili Swahili

Zanzibar Bureau of Standards

ISO 9001: 2015 Certified

Standards | Quality | Life

TAARIFA YA BIDHAA YA MAFUTA YA KUPIKIA YA YALIYO CHINI YA KIWANGO

Zanzibar, 3 Machi , 2022. Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa Sheria ya Viwango ya Zanzibar namba 1 ya mwaka 2011. ZBS imeanza hatua za utekelezaji wa kazi zake rasmi mwaka 2012 ikiwa na jukumu la msingi la kuandaa viwango vya bidhaa na huduma pamoja na kusimamia matumizi ya viwango katika bidhaa na huduma. Lengo kuu la kazi za ZBS ni kulinda afya na usalama wa mtumiaji, kulinda mazingira pamoja na kukuza uchumi wa nchi hivyo katika kuhakikasha hayo ZBS hufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za ukaguzi, uchunguzi wa kimaabara pamoja na uthibiti Ubora.

Katika kutekeleza majukumu yake na kuimarisha mahusiano mazuri na wadau ZBS imekua na utaratibu wa kufanya mikutano mbali mbali na wadau hao wakiwemo wazalishaji na waingizaji wa bidhaa kwa lengo la kutoa elimu na kutatua changamoto zinazowakabili juu ya uzalishaji wa bidhaa zenye viwango na kuweza kuhakikisha kwamba bidhaa zinazozalishwa ndani ya Nchi zinakidhi ubora wa viwango husika pamoja na kupata Udhibiti Ubora wa bidhaa, ZBS baada ya kufanyika uchunguzi wa kimaabara kwa bidhaa mbalimbali za mafuta ya kupikia ilionekana kuna haja ya kukaa na waingizaji na wazalishaji wa bidhaa hii baada ya kugundulika kuwa na sababu iliyopelekea kutokidhi kiwango kwa upande wa parameter ya ‘’Refractive index’’ kwa bidhaa hizo.

ZBS inawasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha bidhaa wanazoingiza zinakidhi matakwa ya viwango husika ili kulinda usalama wa mtumiaji na mazingira yake.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.
S.L.P 1136,
NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225
Barua pepe: info@zbs.go.tz

Previous MKUTANO NA WATAALAMU WA MAZINGIRA