TAARIFA KWA UMMATUJIKINGE NA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU
UNAOSABABISHWA NA KIRUSI CHA CORONA COVID-19
Quality Assurance

Quality products ensure better health and safety for consumers.

Standardization

ZBS facilitates competitiveness and innovation in Global market.

Quality Control


For genuine infrastructures and environmental protection, fullfill the product requirements.
Pre - shipment verification

ZBS ensures imported products comply with the developed Zanzibar and International Standards.

Product Certification
The quality of products depends on the frequent inspection conducted in the manufacturing premises.

Testing

The good art of laboratory, equipment and devices build confidence to traders, consumers and stakeholders.
Training and Consultancy
With full enthusiasm, ZBS is dedicated to grow together with all stakeholders.

    

      TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA WAINGIZAJI WA BIDHAA PAMOJA NA MAGARI YALIYOTUMIKA KUHUSU KUFANYA UKAGUZI WA UBORA WA BIDHAA NJE YA NCHI (PVoC).

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa Sheria ya Viwango ya Zanzibar Nam.1 ya mwaka 2011. Lengo la kuanzishwa ZBS ni kuweka Viwango vya bidhaa na huduma pamoja na kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa Zanzibar zinakua na Viwango na Ubora unaokubalika, ili kulinda afya na usalama wa watumiaji, kulinda mazingira ya Zanzibar pamoja na kukuza uzalishaji wa bidhaa za ubora na kuimarisha biashara nchini.

 

Kutokana na lengo hilo la kuwepo kwa ZBS hapa Zanzibar, bidhaa zote ikiwemo magari yaliyotumika na bidhaa nyenginezo zinazoingizwa nchini zinatakiwa kufanyiwa ukaguzi nje ya nchi kwa kutumia mawakala wa PVoC walioteuliwa na ZBS.

 

Ukaguzi huo utafanywa na Mawakala wetu ambao wanapatikana duniani kote.

 

Mawakala ambao mpaka sasa wamethibitishwa na ZBS kufanya kazi hizi za ukaguzi kwa bidhaa ni:-

1. Société Générale de Surveillance (SGS)

2. Bureau Veritas (BV)

3. China Certification & Inspection Group Co. ltd (CCIC)

 

Aidha kwa upande wa vyombo vya moto vilivyotumika, mawakala waliothibitishwa ni:

1. East Africa Automobile (EAA) kwa gari zote zinazotoka Nchini Japan, Singapore, Hong Kong na Uingereza

 

2. Jabal Kilimanjaro Auto Electric Mechanic. (JKAEM) gari zote zinazotoka Dubai.

 

 

ZBS inawakumbusha waagiziaji wote wa bidhaa na magari yaliyotumika kuhakikisha wanafanya ukaguzi huo kupitia mawakala waliotajwa na kutofanya ukaguzi huo ni kosa na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa waagiziaji watakaohusika.

Waagiziaji wote wanatakiwa kutekeleza taratibu za ukaguzi ili kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kujitokeza.

ZBS inawaomba Waagiziaji na Mawakala wa Waagiziaji kuendeleza ushirikiano katika kufanikisha kazi hii muhimu yenye lengo la kulinda afya na usalama wa watumiaji, kulinda mazingira na kukuza uchumi wa Zanzibar.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-

Mkurugenzi Mkuu

Taasisi ya Viwango Zanzibar

S.L.P 1136

Simu: 255 24 2232225

Nukushi : 255 24 2232225

Barua Pepe: info@zbs.go.tz

Zanzibar

 

Related Link: UTARATIBU WA UKAGUZI WA UBORA WA BIDHAA NJE YA NCHI (PVOC)