TAARIFA KWA UMMATUJIKINGE NA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU
UNAOSABABISHWA NA KIRUSI CHA CORONA COVID-19
Quality Assurance

Quality products ensure better health and safety for consumers.

Standardization

ZBS facilitates competitiveness and innovation in Global market.

Quality Control


For genuine infrastructures and environmental protection, fullfill the product requirements.
Pre - shipment verification

ZBS ensures imported products comply with the developed Zanzibar and International Standards.

Product Certification
The quality of products depends on the frequent inspection conducted in the manufacturing premises.

Testing

The good art of laboratory, equipment and devices build confidence to traders, consumers and stakeholders.
Training and Consultancy
With full enthusiasm, ZBS is dedicated to grow together with all stakeholders.

    

      TAARIFA KWA UMMA

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 1 ya mwaka 2011. Majukumu makuu ya Taasisi hii ni kuandaa Viwango pamoja na kusimamia matumizi ya Viwango hivyo kupitia Ukaguzi, Upimaji na Uthibitishaji Ubora wa bidhaa na Huduma.

Kufuatia kuwepo kwa ugonjwa unaotokana na virusi vya Corona (COVID-19) duniani na hapa nchini, kumekua na matumizi makubwa ya kifaa cha tiba kinga cha vitakasa mikono (Hand Sanitizer) kwa ajili yakunawia mikono kama ilivyo elekezwa na Serikali.

ZBS inapenda kutoa maelekezo na kuwataarifu wananchi kwamba wahakikishe wauzaji na watumiaji kuwa wanauza na kutumia vitakasa mikono (Hand Sanitizer) vilivyothibitishwa ubora wake kupitia Taasisi ya Viwango Zanzibar(ZBS) au Shirika la Viwango Tanzania(TBS) au Viwe vimehakikiwa usalama wake kupitia Wakala wa Chakula Dawa na Vipozi Zanzibar.

Mfanyabiashara yoyote atakaebainika kuuza bidhaa hizo bila ya kupitia katika moja ya Taasisi zilizotajwa hapo juu hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na.1 ya 2011.

Aidha, inasisitizwa wananchi kushirikiana na Taasisi pindi wanapobaini bidhaa hizo ndani ya soko.

Ahsante.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU

TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.

S.L.P 1136,

NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225

Barua pepe: info@zbs.go.tz