TAARIFA KWA UMMATUJIKINGE NA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU
UNAOSABABISHWA NA KIRUSI CHA CORONA COVID-19
Quality Assurance

Quality products ensure better health and safety for consumers.

Standardization

ZBS facilitates competitiveness and innovation in Global market.

Quality Control


For genuine infrastructures and environmental protection, fullfill the product requirements.
Pre - shipment verification

ZBS ensures imported products comply with the developed Zanzibar and International Standards.

Product Certification
The quality of products depends on the frequent inspection conducted in the manufacturing premises.

Testing

The good art of laboratory, equipment and devices build confidence to traders, consumers and stakeholders.
Training and Consultancy
With full enthusiasm, ZBS is dedicated to grow together with all stakeholders.

    

      TAARIFA KWA UMMA

KUANZA KWA UTEKELEZAJI WA MFUMO WA UKAGUZI WA UBORA WA BIDHAA NJE YA NCHI (PVoC)

Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) linapenda kuutaarifu umma pamoja na waagizaji bidhaa wote kutoka nje ya nchi kuwa utekelezaji wa Mfumo wa Ukaguzi wa Ubora wa Bidhaa zote ambazo huingizwa nchini kutoka nje ya nchi "Pre Export Verification of Conformity to Standards" (PVoC) unaanza rasmi kuanzia tarehe 01.11.2016.

ZBS inapenda kusisistiza kuwa waagizaji wote wa bidhaa kutoka nje ya nchi wahakikishe bidhaa hizo zinakaguliwa na kuhakikiwa ubora wake kabla hazijasafirishwa kuja Zanzibar na ziwe zimeambatana na Cheti cha Uthibiti Ubora (CoC).

Kuanzia 01.1.2017 Kwa muagizaji yeyote ambaye bidhaa atakayoingiza nchini Zanzibar na ambayo ikawa haikukaguliwa na kuthibitishwa ubora wake, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kulipa asilimia kumi na tano (15%) ya CIF pamoja na kulipia gharama za ukaguzi wa baada ya bidhaa kufika bandarini hapa Zanzibar kwa mfumo wa "Destination Inspection".

Ikiwa bidhaa hiyo haikukidhi matakwa ya viwango husika, itaangamizwa au kurejeshwa ilipotoka kwa gharama ya mwenye bidhaa hiyo.

Ili kuepukana na usumbufu huu, wanaoagiza bidhaa wote kutoka nje ya nchi wanatakiwa kufanya ukaguzi wa bidhaa zao kabla hazijasafirishwa kwa lengo la kuingizwa nchini.

Ukaguzi huo utafanywa na Mawakala wetu ambao wanapatikana duniani kote.

Mawakala ambao mpaka sasa wamethibitishwa na ZBS kufanya kazi hizi za ukaguzi ni:-

1. Société Générale de Surveillance (SGS)

2. Bureau Veritas (BV)

 

ZBS inawaomba Waagiziaji na Mawakala wa Waagiziaji kuendeleza ushirikiano katika kufanikisha kazi hii muhimu yenye lengo la kulinda afya na usalama wa watumiaji, kulinda mazingira na kukuza uchumi wa Zanzibar. 

 Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-

Mkurugenzi Mkuu

Shirika la Viwango Zanzibar

S.L.P 1136

Simu: 255 24 2232225

Nukushi : 255 24 2232225

E-mail: info@zbs.go.tz

 

Related Link: UTARATIBU WA UKAGUZI WA UBORA WA BIDHAA NJE YA NCHI (PVOC)