TAARIFA KWA UMMATUJIKINGE NA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU
UNAOSABABISHWA NA KIRUSI CHA CORONA COVID-19
Quality Assurance

Quality products ensure better health and safety for consumers.

Standardization

ZBS facilitates competitiveness and innovation in Global market.

Quality Control


For genuine infrastructures and environmental protection, fullfill the product requirements.
Pre - shipment verification

ZBS ensures imported products comply with the developed Zanzibar and International Standards.

Product Certification
The quality of products depends on the frequent inspection conducted in the manufacturing premises.

Testing

The good art of laboratory, equipment and devices build confidence to traders, consumers and stakeholders.
Training and Consultancy
With full enthusiasm, ZBS is dedicated to grow together with all stakeholders.

    

UTARATIBU WA UKAGUZI WA UBORA WA BIDHAA UNAOFANYIKA KABLA YA SHEHENA KUSAFIRISHWA NA KUINGIZWA NCHINI (PVoC).

PVoC (Pre export Verification of Conformity to Standards) ni mfumo wa ukaguzi, uhakiki na uthibiti ubora wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwamba zinakidhi matakwa ya viwango vya kitaifa au kimataifa kabla ya kuingizwa nchini.

 

2.1    Madhumuni na faida za Ukaguzi Ubora wa Bidhaa Kupitia Mfumo wa PVoC.

a.   Kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinakidhi matakwa ya viwango husika kabla ya kusafirishwa.

b.   Kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kuhifadhi mazingira.

c.    Kuongeza ufanisi wa kuondoa pamoja na kupunguza mlundikano wa makasha bandarini.

d.   Kulinda viwanda vya ndani dhidi ya ushindani usio wa haki.

e.    Kwenda sanjari na mageuzi ya teknolojia yanayofanywa na TRA.

f.     Kuzuia Zanzibar isigeuzwa jaa la bidhaa feki na mbovu.

 

2.2            Jinsi utaratibu wa PVoC utakavyotekelezwa.

a.   Mnunuzi wa Zanzibar atawasiliana na muuzaji wake nje ya nchi, atamfahamisha bidhaa anayohitaji na viwango vyake.

b.   Muuzaji atawasiliana na wakala wa huduma za PVoC aliyepo karibu nae ili apate utaratibu wa kufuata kabla ya kusafirisha shehena.

c.    Wakala wa PVoC atakagua pamoja na kupima bidhaa husika na kutoa Cheti cha Ubora “Certificate of Conformity” (CoC)  endapo bidhaa hiyo itakidhi matakwa ya viwango husika.

d.   Wakala wa PVoC atatuma CoC halisi (original) kwa mnunuzi aliyeko Zanzibar na nakala ya CoC itatumwa kwa muuzaji.

e.    Mnunuzi atawasilisha CoC halisi ZBS kwa uhakiki na ZBS itatuma CoC hiyo TRA kwa njia za elektroniki ili kuruhusu bidhaa kutolewa bandarini.

f.     ZBS itafanya ukaguzi kwa wakala wa PVoC mara kwa mara ili kuhakikisha kazi imefanyika kulingana na mkataba.

 

 

3.0    NJIA/MIFUMO YA UKAGUZI (INSPECTION ROUTES)

Bidhaa zinazokaguliwa kwa mfumo huu zinaweza kusafirishwa kwa kupitia njia (Route) kuu tatu kutegemeana na aina ya msafirishaji husika.  

 

I.      Njia A (Route A): Ukaguzi pamoja na kupata cheti cha ubora.

Katika njia hii, bidhaa inayosafirishwa ni lazima ikaguliwe na ipimwe maabara  ili kuhakikisha kwamba bidhaa inakidhi viwango husika.

Njia hii inahusu bidhaa zote ambazo zinasafirishwa na wafanyabiashara au watengezaji wa bidhaa.

 

Hatua za kupata Cheti cha Uthibiti Ubora kupitia njia A ni kama zifuatazo:

Ø  Msafirishaji wa bidhaa hupeleka maombi ya kupatiwa Cheti cha Uthibiti Ubora kwa wakala wa PVoC.

Ø  Wakala wa PVoC atapitia  na kuhakiki maombi na nyaraka zote muhimu zilizowasilishwa na muombaji.

Ø  Mkaguzi wa ubora atakagua shehena inayotaka kusafirishwa pamoja na kuchukua sampuli.

Ø  Sampuli kupelekwa maabara kwa ajili ya upimaji.

Ø  Wakala wa PVoC atatoa Cheti cha Uthibiti Ubora  ikiwa bidhaa imekidhi viwango.

 

II.     Njia B (Route B): kusajili bidhaa pamoja na kupata Cheti cha Uthibiti Ubora.

Hii ni njia ya uhakika na ya haraka katika upatikanaji wa Cheti cha Uthibiti Ubora. Katika njia hii, bidhaa inayosafirishwa kuletwa nchini husajiliwa na wakala wa PVoC katika nchi husika.

Msafirishaji wa bidhaa anashauriwa kusajili bidhaa yake ya aina moja (Homogeneous Product) ambayo mara nyingi husafirisha na kuingiza nchini.

Hatua za kusajili bidhaa pamoja na kupata Cheti Cha Uthibiti Ubora kupitia njia B ni kama zifuatazo:

 

a) Kusajili bidhaa inayosafirishwa

· Msafirishaji wa bidhaa anatakiwa kupeleka maombi ya   kusajiliwa bidhaa yake kwa wakala wa PVoC.

· Wakala wa PVoC atahakiki na kupitia nakala zote za muombaji kabla ya kuisajili bidhaa yake.

b) Kupatiwa Cheti cha Uthibiti Ubora kwa bidhaa iliyosajiliwa:

·       Kupeleka maombi ya kupatiwa Cheti cha Uthibiti ubora kwa Wakala wa PVoC.

·       Mkaguzi kwenda kukagua shehena inayotaka kusafirishwa pamoja na kuchukua sampuli.

·       Sampuli kupelekwa maabara kwa ajili ya upimaji.

·       Wakala wa PVoC kutoa Cheti cha Uthibiti Ubora ikiwa bidhaa imekidhi viwango.

 

III.    Njia C (Route C): Kusajili bidhaa pamoja na kupatiwa cheti cha Uthibiti Ubora kwa shehena inayosafirishwa.

}  Njia hii inatumika kwa wazalishaji wakubwa ambao wanatumia mfumo bora wa usimamizi katika uzalishaji wao (Quality Management System).

}  Katika mfumo huu, wakala wa PVoC atahakiki mfumo mzima wa uzalishaji wa kiwanda cha mzalishaji huyo.

}  Njia hii inapendekezwa kwa wazalishaji ambao wanasafirisha shehena kubwa ya bidhaa.

 

a) Hatua za kupata leseni ya uthibiti ubora katika Njia C

Ø  Msafirishaji wa bidhaa kupeleka maombi ya kupatiwa leseni ya Ubora kwa wakala wa PVoC.

Ø  Wakala wa PVoC kuhakiki maombi ya msafirishaji wa bidhaa.

Ø  Kupimwa bidhaa ili kuhakikisha kwamba bidhaa inaendana na viwango husika.

Ø  Ukaguzi wa mara kwa mara baada ya mzalishaji kupatiwa leseni ya ubora.

Ø  Leseni hii ya ubora itatumika kwa muda wa mwaka mmoja.

b) Bidhaa yenye leseni ya Ubora kupatiwa Cheti cha Uthibiti Ubora.

Ø  Shehena inayotaka kusafirishwa kukaguliwa na mkaguzi husika wa ubora wa viwango.

Ø  Bidhaa baada ya kukaguliwa haitopimwa maabara.

Ø  Msafirishaji kupewa Cheti cha Uthibiti Ubora (CoC)

 

Gharama za Ukaguzi katika Mfumo wa PVoC

NJIA

% FOB

GHARAMA YA CHINI (USD)

GHARAMA YA JUU (USD)

A

0.53

250

3000

B

0.45

250

3000

C

0.25

250

3000

 

4.0   Bidhaa ambazo zitakaguliwa kupitia mfumo wa PVoC kuanzia 1 Novemba, 2016.

Kundi la kwanza:  Vitu vya kuchezea watoto (Toys).

Kundi la Pili:  Vifaa vya umeme na elektroniki ikiwa pamoja na vifaa vya umeme wa jua.

Kundi la tatu: Vifaa vya vyombo vya moto .

Kundi la nne: Bidhaa za kemikali ikiwa pamoja na vipodozi.

Kundi la tano: Vifaa vya ujenzi pamoja na vya mekanika kama vile, nondo, paipu, mabati ya kuezekea n.k.

Kundi la sita: Vyandarua.

Kundi la Saba: Samani za majumbani na maofisini (furnitures) ikiwa za mbao au za chuma.

Kundi la nane: Karatasi pamoja na vifaa vya kuchapishia.

Kundi la tisa: Vifaa vya usalama na kujikinga.

Kundi la kumi: Vyakula na bidhaa zinazotokana na vyakula.

Kundi la kumi na moja: Vyombo vya moto vilivyotumika.

 

4.1    Bidhaa zilizosamehewa kufanyiwa Ukaguzi kupitia mfumo wa PVoC.

·       Bidhaa ambazo mzigo wake hauzidi Dola 1000.

·       Bidhaa zilizopigwa marufuku kwa mujibu wa Sheria ya “Customs Management” ya Afrika Mashariki  na Sheria ya Afrika Mashariki ya Viwango, Uthibiti Ubora na Uchunguzi wa kimaabara (SQMT 2006).

·       Mizogo midogo ya mtu binafsi.

·       Bidhaa ambazo zina Alama ya Ubora ya Zanzibar na zile zote zilizothibitishwa ubora wake ndani ya Afrika Mashariki, mfano Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi.

 

Mawakala ambao mpaka sasa wamethibitishwa na ZBS kufanya kazi hizi za ukaguzi ni:-

1. Société Générale de Surveillance (SGS)

2. Bureau Veritas (BV)