TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ADHABU (PENALTY) YA ASILIMIA 15 CIF KWA KUTOFANYA UKAGUZI WA UBORA WA BIDHAA NJE YA NCHI (PVoC) KUANZIA TAREHE 1 SEPTEMBA, 2017
Taasisi ya Viwango (ZBS) imeanzishwa kwa Sheria ya Viwango ya Zanzibar Nam.1 ya mwaka 2011. Lengo la kuanzishwa ZBS ni kuweka Viwango vya bidhaa na huduma pamoja na kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa Zanzibar zinakua na Viwango na Ubora unaokubalika, ili kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kulinda mazingira ya Zanzibar.
Kutokana na lengo hilo la kuwepo kwa ZBS hapa Zanzibar, bidhaa zote zinazoingizwa nchini ni lazima zihakikishwe ubora wake kupitia mfumo wa Ukaguzi wa Ubora wa Bidhaa Nje ya Nchi (PVoC). Aidha, bidhaa zote ikiwemo magari na bidhaa nyenginezo zinazoingizwa nchini zinatakiwa kufanyiwa ukaguzi nje ya nchi kwa kutumia mawakala wa PVoC walioteuliwa na ZBS.
Taasisi ya Viwango Zanzibar ZBS inatoa taarifa Rasmi ya kuanza Utekelezaji wa Adhabu ya asilimia 15 ya CIF kuanzia tarehe 01 Septemba, 2017 kwa bidhaa zote zitakazoingizwa nchini bila ya kufuata utaratibu wa Ukaguzi wa Bidhaa Nje ya Nchi (PVoC).
Ukaguzi huo utafanywa na Mawakala wetu ambao wanapatikana duniani kote.
Mawakala ambao mpaka sasa wamethibitishwa na ZBS kufanya kazi hizi za ukaguzi ni:-
1. Société Générale de Surveillance (SGS)
3. China Certification & Inspection Group Co. ltd (CCIC)
4. East Africa Automobile (EAA)
5. Jabal Kilimanjaro Auto Electric Mechanic
ZBS inawaomba Waagiziaji na Mawakala wa Waagiziaji kuendeleza ushirikiano katika kufanikisha kazi hii muhimu yenye lengo la kulinda afya na usalama wa watumiaji, kulinda mazingira na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-
Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Zanzibar
S.L.P 1136
Simu: 255 24 2232225
Nukushi : 255 24 2232225
E-mail: info@zbs.go.tz
Related Link: UTARATIBU WA UKAGUZI WA UBORA WA BIDHAA NJE YA NCHI (PVOC)